Zifuatazo ni fasili za maneno yanayotumika nchini Canada katika mazungumzo ya baraka zinazohusu usenge na jinsia za aina moja.

Usenge: (Kamusi ya Oxford ya Canada-KOC¹): “1 hisia za au kuhusika  na kuvutiwa kijinsia na watu wenye jinsia ya aina moja. 2. kuhusu uhusiano wa kisenge au watu

3. kuhusu jinsia ya aina moja. Nomino. msenge.”

Msagaji: (KOC): “Nomino: mwanamke ambaye anavutiwa kijinsia na wanawake wengine. Kivumishi cha au  kinachohusiana na wasagaji.”

Huntha: (KOC): “kivumishi. 1. anayevutiwa kijinsia na watu wa jinsia zote mbili. 2.

-a kibiolojia. Yenye  tabia za jinsia zote mbili. 3. ya au inayohusu jinsia zote mbili. Nomino. huntha.

Msenge: (KOC): “kivumishi. 1a  -a kisenge; b  inayohusu wasenge. Matumizi ya neno msenge yaani “gei” kumaanisha msenge linapendelewa na wasenge, na hivi sasa limeimarishwa na kutumika kote katika matumizi ya kawaida. Mara nyingi linawahusu   wasenge wanaume na kufautisha na msagaji wakati wa kuzungumzia juu ya wasenge kama jamii.”

Mwelekeo wa kijinsia: (KOC): “nomino. jambo la kuvutiwa na watu wa jinsia tofauti na jinsia ya mhusika, au jinsia zote mbili.” Kuna mazungumzo yanayoendelea kati ya wataalam kuhusu chanzo cha mwelekeo wa kijinsia za mtu. Baadhi ya ushahidi unaonyesha kuwa asili yake ni sababu za kibiolojia /kijenetiki; uchunguzi mwingine  unaonyesha athari za kijamii. Mazungumzo ya hivi karibuni yanaeleza kwa muhtasari sababu zisizoeleweka kwa urahisi zinazochangia katika kusababisha asili ya mwelekeo wetu wa kijinsia katika mwendeleo wa wakati.

Ndoa: Aina tatu za Ndoa:

Kamusi: (KOC): “nomino. 1. muungano wa  kisheria au dini kati ya mwanaume na mwanamke kwa madhumuni ya kuishi pamoja na mara nyingi kuwa na watoto. 2. kitendo au sherehe za kuanzisha muungano huo.”

Sheria iliyopendekezwa C-38: Serikali ya Canada: (Hivi sasa mswada uko katika Bunge  la Canada). “Ndoa kwa ajili ya madhumuni ya kiraia, ni muungano wa kisheria kati ya watu wawili ukiondoa wengine wote.”

Kanisa la Kianglikana la Canada: Mkutano wa Sinodi Kanuni XX1: “Kanisa la Kianglikana la Canada linathibitisha ,…., kwamba ndoa ni muungano wa maisha katika mapenzi ya kuaminiana, na kwamba viapo vya ndoa ni ahadi kwa muungano huo, kwa mazuri au mabaya, kwa kuondoa wengine wote katika pande zote mbili. Muungano huo umeanzishwa kwa upendo wa Mwenyezi Mungu wakati watu wawili wennye sifa zinazotakiwa wanapojiunga katika mkataba wa ndoa ambapo wanatangaza nia yao ya kutimiza madhumuni yale na kubadilishana viapo vya kuaminiana mpaka hapo watakapotenganishwa na kifo. Madhumuni ya ndoa ni maafikiano ya pande zote mbili, ushirikiano, kusaidiana, kufajiriana, na kuzaa (kama itakuwa hivyo) na malezi ya watoto, na uanzishaji wa uhusiano ambao ujinsia unaweza kutumika katika kukamilisha haja ya mtu binafsi katika jamii ya mapenzi ya kuaminiana. Mkataba huu unafanywa mbele ya Mwenyezi Mungu  na kushuhudiwa na mashahidi na mchungaji aliyeidhinishwa.”

Baraka: (Kutoka katika Kitabu cha Sherehe za Mara Chache-Kanisa la Kianglikana la Canada, 1992).

“Tunawabariki watu si kwa sababu ya kuongeza hadhi yao ya kiroho bali kutoa shukrani kwa nafasi walizoteuliwa kuzifanya katika utawala wa Mwenyezi Mungu na kwa hiyo kuwaachia katika kutoa mchango wao…. Kwa karne kadhaa Kanisa limewabariki watu, maeneo, na vitu, licha ya sherehe za ekaristi takatifu, na jambo hili ni sawa kabisa ili mradi mazingira ya Kiekaristi katika maisha yote ya Kanisa yanakumbukwa. Kila sala ya baraka ni shukrani kwa uumbaji na ukombozi inapotolewa katika ombi kwa ajili ya kutimizwa kwa madhumuni matakatifu ya watu wa Mwenyezi Mungu na kwa ulimwengu wote. Kama ilivyo Ekaristi yenyewe, sala za baraka ni marejeo ya mwanga uliochepuliwa kwenda kwenye chanzo chake. Daima baraka ni nyongeza na matumizi ya sala kuu ya kanisa.

Baraka ya jinsia ya Aina moja:  (Kanisa)

Kutoka katika Ripoti ya Mtakatifu Michael (Kamisheni ya Kitheolojia ya Askofu Mkuu, Kanisa la Kianglikana la Canada, Mei, 2005):

Kamisheni inaelewa istilahi “muungano wa ahadi ya jinsia ya aina moja” kuwa na maana ya iliyoahidiwa, ya kiutu uzima, ndoa moja, yenye madhumuni ya maisha, uhusiano wa jinsia ya aina moja ambayo inajumlisha kujamiliana kijinsia.

Muungano wa Kiraia: ahadi kati ya watu wawili wa jinsia ya aina moja mmoja kwa mwengine kama inavyotambuliwa na viwango vya kisheria vya mahali panapohusika. Watu wawili wanaweza kuunganishwa katika muungano wa kisheria unaotambuliwa katika majimbo kadhaa nchini Canada kwa wakati huu.

Mseja: (KOC): “1. aliyeahidi kuepukana na mahusiano ya kijinsia na ndoa, hasa kwa sababu za kidini. 2. kuepukana na mahusiano ya kinjinsia.” Wanachama wa mashirika ya kidini  wanakula viapo vya kutooa ikiwa kama ni sehemu ya ahadi yao kwa maisha ya jumuiya ya Kikristu, wakiyaona kama ni sehemu ya wito wa kazi yao. Watu wengine wanaweza kuishi katika hali ya kutooa ikiwa kama ni mahitaji ya jamii kabla ya ndoa, lakini hawaoni kama hali hii ni wito wa kudumu. Kanisa linategemea kwamba wale ambao hawaoi au kuolewa wanabaki kuwa waseja.

Kanisa la Kianglikana la Canada

¹ Vipengele vilivyoonekana (KOC): Kutoka katika  Kamusi ya Oxfod ya Canada. Haki ya kunakili 1998, 2004

Oxford University Press

Links: